VIFO VYA WAZAZI WANGU VYANITIA UCHIZI
Ilikuwa ni siku ya mwisho mwa juma {jumapili} nikiwa mimi na baba yangu tulikuwa tukielekea maeneo ya tandale kumtembelea rafiki yake baba ambaye walikuwa wakifanya kazi pamoja. Baba yangu alikuwa akipenda sana kuwa karibu nami kwa kuwa mimi ndiye niliyekuwa mtoto wake wa kike pekee katika familia ya watoto wanne.
Hata nami nilikuwa nikijisikia fahari kuwa karibu na baba yangu na kutembea nae pale anapohitaji. Lakini tukiwa njiani kuelea kwa rafiki wa baba ambaye alikuwa anaitwa Sajali tulikutana na umma wa watu waliokuwa wakishangilia na kuchochea uogomvi kati ya vijana wawili waliokuwa wakigombana. Nilitamani nikawagolezee lakini sikuweza kufanya hivyo kwakuwa nilikuwa sina nguvu ya kuwatawanyisha watu waliokuwa wamewazunguka vijana waliokuwa wakigombana.
Tuliachana na kushangaa tukio hilo kisha tukawa wenye kuendelea na safari yetu. Tulipofika maeneo ya tandale kwa mtogole simu ya baba ilikuwa inaita hivyo ilimbidi aitoe mfukoni kwa ajili ya kuwasiliana. Wakati anatoa simu yake kutoka katika mfuko wa suruali alitokea kijana mmoja na kumgusa bega la kushoto kwa kuashiria kama anamuita.Baba alivyogeuka upande ule wa kushoto ghafla alitokea mtu kwa upande wa kulia na kupola simu ya baba kisha akawa anakimbilia sehemu za vichochoroni. Baba hakutaka kukubali kwa kunyang'anywa simu yake hivyo ilimbidi awakimbize wezi waliomuibia simu yake huku akipiga kelele za wizi.
Kutokana na tukio lililotokea nilipatwa na bumbuwazi {mshangao} nakushindwa kufanya maamuzi ya haraka, baada ya mda kidogo nami nilielekea upande uleule aliokuwa akikimbilia baba alipokuwa akiwakimbiza wale wezi wa simu.
Lakini kilichonistaaajabisha hakuna mwananchi aliyekuwa akitoa msaada kwa wakati ule ispokuwa walikuwa wakiendelea kufanyanya shughuli zao.Nilipofika mbele kidogo niliona baadhi ya watu wakijitokeza na kushangaa lile tukio. Wasiwasi ulinishika kwa kuwa sikuwa mwenye kujua nini kinaendelea kati ya baba yangu na wale wezi wa simu. Mara nilisikia kelele za watu wakiitia mwizi kwa upande wa mbele nilipokuwa nikielekea. Ilinibidi niongeze kasi ili nikamsaidie baba yangu.Kumbe zile kelele za wizi nilizokuwa nikizisikia ni wale wezi wa simu wakiwa na wahuni wenziwao walimgeuzia kibao baba yangu na kumuitia kelele za wizi huku wakimtupia mawe.
Baba yangu aliona njia pekee ya kujitetea ni kukimbilia maeneo ya barabani, masikini mzazi wangu kumbe kukimbia kwake baadhi ya wananchi wenye hasira kali walifikiri yule ndiye mwizi aliyekuwa ameiba simu.
Hivyo kundi la watu lilimzonga na kuanza kumpiga kwa mawe na magongo. Nilijitahidi kumsaidia baba yangu kwakupiga kelele na kuwaeleza wananchi huyo siyo mwizi bali wamemsingizia lakini hakuna hata mtu mmoja aliyenisikiliza kinyume chake kichapo kiliongezeka kwa upande wa baba yangu.
Haikuwa rahisi kuamini kile nilichokuwa nikikiona nakuhisi kama mtu niliyekuwa usingizini nikiota. Na kila nilipokuwa nikiomba msaada kwa watu wanisaidie hakuna hata aliyekuwa akinijali. Kutokana na hali hiyo ilipelekea niishiwe nguvu huku nikiwa nalia kwa hasira na machungu makali ya unyama waliokuwa wanaufanya wezi wale.
Baada ya mda askari walipata taarifa hivyo walisogea hadi eneo la tukio kwa lengo la kumkamata muharifu. walimshika baba yangu wakiwa wamembeba na kumpakia katika gari yao. Nilipoangalia pale chini niliona damu imemwagika kwa kiasi kikubwa na kutapakaa eneo la tukio.
Nilirudi nyumbani huku nikiwa nalia njia nzima, nilipofika nyumbani walishangaa kuniona peke yangu kisha huku nikiwa nalia. Ilinibidi niwaelezee kile kilichotokea, Baada ya kujua kilichotokea wote tukawa tunalia huku tukiwa tunaelekea hospitali ya taifa Muhimbili kwa lengo la kujua hali ya baba yangu inaendeleaje.
Kweli tulifanikiwa kufika hospitalini na kujaribu kumuulizia mzazi wetu hodi aliyolazwa. Baada ya kuuliza tulipokea tarifa kuwa hali ya baba yetu ilikuwa mbaya sana na amelazwa katika chumba cha I C U. Pamoja na hayo hatukuwa wenye kukata tamaa hivyo tulikaa na kusubiri nini kitakacho endelea kwa upande wa mgonjwa wetu.
Baada ya muda kidogo kupita alikuja daktari na kutaka azungumze na mkubwa kutoka katika familia yetu. Hivyo kwa mda ule alijitokeza kaka yetu wa kwanza kwa kuwakilisha familia nzima. Mara baada ya mazungumzo kuisha baina ya daktari na kaka yetu tulimuona kaka akirejea huku machozi yakimtoka na akiwa na huzuni kubwa. Tulivyomuuliza daktari anasemaje kuhusu mgonjwa wetu, alitujibu kwa sauti ya chini na upole huku akisema baba ameshafariki.
Baada ya kupokea taarifa hiyo ghafla mama alianguka chini kutokana na presha aliyonayo. Hivyo ilibidi baadhi ya watu watusaidie kumchukuwa mama yetu na kumpeleka kwa daktari kwa ajili ya matibabu.
Kiukweli maamuzi ya mungu ni mazito tena ni makubwa. Kwa maana mda ule ule tukapewa taarifa kuwa mama yetu naye ameiyaga dunia kutokana na mshtuko alioupata.Kitu ninachoamini kazi ya mola huwa haina makosa. Pia sikuwahi kufikiria kutokana na hayo yaliyotokea kwa kudhani kulikuwa na mkono wa mtu ispokuwa ni mitihani tu ya mola wangu.
Namuomba mwenyezi awalaze mahali pema wazazi wangu.
Category: MY DIARY







Daah! ebana pole sana kwa yaliyokukuta
ReplyDelete