ULEVI NDIYO ULIONIFANYA NIZARAURIKE
Katika maisha yangu sikuwahi kufikiria kuwacha pombe kwakuwa sikuona starehe itakayo nifaa zaidi ya pombe.Wapo wengi niliokuwa nikiwakwaza kutokana na tabia yangu ya ulevi hususa ni wazazi wangu pamoja na ndugu zangu. Kwakuwa nilisha athiriwa na tabia hiyo, ilifika kipindi mpaka sikuona hata umuhimu wa kuwa na mke nakuhisi starehe pekeekwangu ni pombe. Kilichonifanya niache pombe ni hiki:-
Nakumbuka siku moja nililewa sana kiasi ambacho hata kutembea nilikuwa nashindwa, mbaya zaidi ilikuwa ni mida ya saa sita za usiku. Hivyo nilikuwa nikijikokota kuelekea nyumbani kwa ajili ya kupumzika. Lakini sikufanikiwa kufika nyumbani kwa usiku ule kutokana na hali niliyokuwa nayo hivyo nilijikuta nimeanguka chini na kupitiwa na usingizi.
Asubuhi nilivyoamka pombe ilikuwa imeshanitoka hivyo ilinibidi nisimame na kutaka kuanza safari yangu. Kabla sijaondoka eneo lile niliisi kuna utofauti mkubwa katika mwili wangu. Tofauti hizo niliziona hasa sehemu za makalio yangu kwakua kulikuwa kama na majimaji yenye kuteleza. Nilivyojikagua vizuri niliweza kujua yale majimaji yalikuwa ni manii. Hivyo niliweza kubaini kuwa kipindi kile nilichokua nimelala kuna watu walikuja na kuniingilia kinyume na maumbile. Nguvu za miguu ziliniishia ghafla na kuketi chini kwa mda, lakini niliona bora nijikokote na kuelekea nyumbani ili watu wengine wasije kujua kilichonikuta.
Siku nzima nilishinda ndani huku nikiwa na mawazo juu ya tukio nililofanyiwa. Hali hiyo ilinifanya nibadilike na kumrudia mungu wangu na kuachana kabisa na masuala ya pombe.
Baada ya mwezi kupita wadogo zangu wa kiume walikuwa wakijisifia mbele yangu kuwa wao ndiyo walionifanyia mchezo ule wa kunilawiti. Tena walisema tumefanya vile kwa makusudi ili niache pombe. Roho iliniuma sana na nilitamani hata kuwa uwa ndugu zangu. Lakini kadri mazungumzo yalivyokuwa yakiendelea waliniambia ukweli kuhusu tukio lile, kuwa hakuna walichonifanya ila walinimwagia majimaji ya mayai ambayo yanafana na manii.
Sikuamini kwa waliyoyasema lakini ilinibidi ni kubaliane nao kwakuwa sikuwahi kumsimulia yeyote kuhusu yakiyonikuta ila waliniona nimeacha pombe ghafla tu. Sikutaka kuwalaumu kwa walichokifanya ila niliwashukuru kwakuwa ilikuwa kama dawa ya kuacha ulevi kwa upande wangu.
Category: MY DIARY







0 comments:
Post a Comment