BOMOA BOMOA YALETA VILIO
Wakazi wa tandika maeneo ya devis kona wavunjiwa nyumba. Baadhi ya wafanya biashara waliokuwa wamepanga katika nyumba zilizovunjwa waingia hasara. Tukio hilo lilifanyika kwakuwa wenye nyumba hao walikuwa wameshalipwa pesa na serikali lakini walivyoona serikali imekaa kimya kwa mda mrefu kidogo wakaisi watakuwa wamejisahau. kutokana na sababu hiyo wananchi hao waliendelea kukaa na kupangisha nyumba zao. Ila siku ya vunjavunja ilipofika imewahadhili. Lakini pia siku hiyo ilikuwa neema kwa mateja kwani walikuwa wakisaidia bomoa bomoa ili nao wapate kuondoka na mali za wafanyabiashara.
Category:

















