Tuesday, April 1, 2014

HAYA NI MAONI YA WANANCHI WA KAWAIDA KUTOKANA NA MTAZAMO WAO

Tunashukuru viongozi mbalimbali walioko serikarini na taasisi tofauti tofauti za kidini kwa kupigania haki za kina mama. Pia tunawapongeza hata wakina mama kwa kuliewa jambo kama hili na kuendelea kulitilia mkazo ili kupata usawa baina ya mwanamume na mwanamke. Tena tunasema hongera hata kwa wale waliothubutu kuanzisha vyama au taasisi maalumu zinazo simamia haki za wanawake.
Lakini pia sisi ambao tuko mtaani tunafahamu na kuelewa kuwa lengo kuu la kuanzishwa taasisi au vyama vya wanawake Tanzania kama UWT, MEWATA,TAWLA na vyenginevyo ilikuwa ni kutetea na kupigania haki za wanawake dhidi ya unyanywasaji wa kijinsia na udhalilishwaji uliokuwa ukifanyika kwa upande wa wanawake.
Tunaamini pia taasisi au vyama hivi mpaka kufikia sasa vimefanikiwa kwa kiasi fulani kuweza kuleta mabadiliko na usawa kati ya wanawake na wanamume. Na kitu ambacho kimepelekea kuleta athari kwa upande wa wanawake kama tunavyoshuhudia sasa baadhi ya wanawake wengi hujipa kipao mbele katika kuthubutu kugombania ngazi mbalimbali za uongozi serikalini.
Lakini tuna wasiwasi na mashaka makubwa  kwa kujiuliza maswali yasiyokuwa na majibu sahihi. Kwa mfano miongoni mwa maswali yetu ni kwamba hizi taasisi au vyama hivi vimeanzishwa kwa lengo la kupigania haki za kina mama dhidi ya udhalilishwaji, unyanywasaji na kutaka kumfanya mwanamke apate heshima yake kama watu wengine au taasisi hizi na vyama hivi vimeanishwa kwa lengo na maslahi ya watu fulani???
Tunasema hayo kwakuwa bado tunaona huyu mwanamke aliyekuja kukombolewa na taasissi/vyama hivyo bado anadhalilishwa tena kwa kutembezwa akiwa nusu uchi/uchi kabisa mbele ya hadhara ya watu. Tena cha kusikitisha huwa wanafanya matendo hayo mbele ya watu wazima kama wazazi wao, ni aibu ilioje...??
Tena hupewa majina mazuri kwa kuitwa walimbende(miss) na wanyewe wameridhika kufanya jambo hilo ni kama ajira au njia ya kujiingizia kipato kwa namna moja au nyingine.pia hata baadhi ya viongozi wa kiserikali hualikwa na kuudhuria katika matamasha hayo bila ya wasiwasi.

Embu tazama picha hizi kisha tujiulize je ni kweli taasisi/vyama hivi vimeweza kupinga udhalilishwaji dhidi ya wanawake???


 


Kutokana na ufinyu wa kimawazo kwetu sisi tunaona bado taasisi/vyama hazijafanikiwa katika baadhi ya mambo. Hivyo tunapenda kuzishauri taasisi husika kuendelea kupigania haki za msingi za kina mama bila kubagua, na kama watakusudia kwa dhati watafanikiwa kinyume chake ni kufeli.



0 comments:

Post a Comment