Tuesday, April 1, 2014

NEWS

ONYO
Hii ni kwa wale wanaopenda kukaa na watoto wa watu bila ya kufunga nao ndoa


Kijana mmoja alikua akiishi na msichana ambae kabila lake ni mgita kwa mda wa takribani miaka minne bila ya kumuona na kuishi nae kama mke na mume. Alijikuta analipishwa mahali baada ya msichana aliokuwa akiishi nae kufariki. 
Mzozo ulikuwa siku ya mazishi ya binti huyo ambapo baba mzazi wa msichana yule alimwambia mkwewe atoe faini ya shilingi milioni moja kwakua alikaa na binti yake bila ya kumuoa. Na aliendelea kwa kusema kama akishindwa kulipa pesa hiyo basi maiti hile haitozikwa. Ndugu kwa upande wa mume ilibidi waende kumtaka radhi mzazi huyo ili wazikea.Lakini mzazi huyo alikataa  kabisa na huku akiendelea kudai fedha hizo. Wanandugu kwa upande wa mwanaume ilibidi wamuombe mzee huyo japo wampatie shilingi laki nne badala ya kulipa milioni moja.Baada ya wanandugu wale kuomba kwa mzee huyo, yule mzee alikubali na ndipo mazishi yakafanyika.

0 comments:

Post a Comment