Tuesday, April 1, 2014

MY DIARY

JOGOO LANGU HALIWIKI 


Leo tupo na bwana Ally ambaye aliweza kusimulia miongoni mwa matatizo aliyowahi kuwa nayo kama ifuatavyo-:

Kwa jina ninaitwa Ally Zola ni kijana mwenye umri wa miaka ishirini na tano {25}. katika maisha yangu hakuna kitu kilichokuwa kinaninyima raha kama kudharaurika na kuonekana kama mtu dhaifu na nisiyekuwa na faida kwa kuumbwa mwanaume eti kwasababu ya mitihani tu ya kimaradhi.

Nakumbuka nilipokuwa na umri wa miaka ishirini {20} nilipatwa na mtihani wa jogoo langu kutowika kabisa kitu ambacho kilikuwa kina ninyima raha na kukosa amani katika maisha yangu. tatizo hili sikuweza kujua ni nini chanzo chake kwani lilinikuta katika mazingira nisiyo ya elewa. kitu ambacho kilinipelekea kuwa na msongo wa mawazo kwa kipindi cha mda mrefu bila ya kujua nianzie wapi kufanya utatuzi wa tatizo langu, hofu yangu kubwa ilikuwa endapo watakapo kuja kujua marafiki zangu kama nimekuwa hanithi niliisi watanifikilia vibaya na hata kunidhania labda nimekuwa shoga.

Hivyo kutokana na hofu hiyo niliyokuwa nayo ilipelekea kudumu na tatizo hilo kwa mda wa miaka miwili bila ya mtu yeyote kujua nasumbuliwa na nini. Lakini nilipofikisha umri wa miaka ishirini na tatu nilishindwa kuvumilia hali hii nikaona bora nianze kutafuta na kuomba ushauri kwa watu wasionijua. Kweli nilipata ushauri tofauti tofauti kutoka kwa watu mbalimbali. Miongaoni mwao walinishauri nitumie baadhi ya miti shamba na wengine walinishauri nijaribu kutumia sana mchuzi wa pweza. kama unavyojua mtu unapokuwa na shida huwa auchagui wa kukusaidia na hata baadhi ya ushauri utakaopewa ili mradi tu ufanikiwe kutatua tatizo lako.

Baada ya kusota kwa mda mrefu bila ya kupata ufumbuzi wa tatizo langu nilikutana na bwana steve ambaye alijaribu kunishauri nikamuone daktari huenda akanisaidia. Nami wala sikupuuzia na kama alivyo nishauri bwana Steve ndivyo nilivyofanya.  Nashukuru nilipo onana na daktari nilimuelezea tatizo langu nae akanipa orodha ya vitu vinavyosababisha tatizo hili.

Alinambia "Uhanithi unawezwa kusababishwa na mambo yafuatayo:-
1. Karibu 50% ya watu wenye tatizo hili husababishwa na umri, msongo wa mawazo n.k.
2. Magonjwa sugu katika mwili, kwa mfano, ugonjwa wa figo, kisukari, kifua kikuu n.k.
3. Matumizi yaliyokithiri ya dawa za kulevya na pombe.
4. Pia vyakula vya mafuta kwani huweza kusababisha mrundikano wa mafuta katika mishipa ya damu na kusababisha mishipa ya damu kushindwa kufika vizuri katika uume ili kuuwezesha kusimama.

Baada ya kujua hayo nilifurahi kidogo na kuwa na hamu pamoja na shauku ya kutaka kujua kama tatizo hili linaweza kutibika au laa.
Daktari alinijibu kwa kusema "kitu cha msingi ni kujua chanzo cha tatizo husika". Na endapo kitakapo bainika chanzo basi utatuzi wake utakuwa rahisi.   Lakini suala la msingi daktari aliniuliza je katika sababu nilizozitaja kuhusu tatizo hili je umeshajua chanzo au sababu ya tatizo lako?  Nilikaa kimya kidogo kwa kufikiri kisha nikamwambia miongoni mwa sababu ulizozita ambazo husababisha tatizo hili mimi nimeangukia katika ulevi wa pombe kupita kiasi.

Baada ya kumueleza hayo daktari aliweza kunishauri na kitu cha kufanya  ili niweze kutatua tatizo langu. Kweli mungu si athumani baada ya kufuata maelekezo ya daktari   kwa muda fulani nilianza kurudisha hali yangu ya kawaida na kupona kabisa na mpka sasa ninamshukuru Mungu nina mke na watoto wawili.    

0 comments:

Post a Comment