This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Sunday, April 20, 2014

LAANA TUPU
Tazama hawa watoto wakike wakilana uroda wao kwa wao, ama kweli ulimwengu tuliokuwa nao si mzuri. Hivi ni kweli wanachokifanya mabinti hawa ni sahihi..?? 
Haya ndiyo mambo ya walimwengu.

SIKIA HII KUTOKA KWADOGO JANJA;
Dogo: Mhudumu niletee bia
Mhudumu: nikuletee chupa ngapi?
Dogo: Kwanza niletee chupa kumi
Mhudumu: Sawa naleta
dogojanja baada yakupiga bia zake akawa anasepa taratibuu


Mhudumu: Kaka tunaomba ulipe pesa za bia ulizokunywa
Dogo: Kwani wewe ujasikia kwenye redio kama watoto tunatakiwa kupewa bia bure kwakua haziruhusiwi kuuzwa kwa wenye umri chini ya miaka kumi na nane?
Mhudumu: Eeenhe!!!




MANCHESTER UNITED YAKALISHWA NA EVERTON BAADA YA KUPEWA KICHAPO CHA MABAO MAWILIBILA

      2-0     

LIVER POOL YATUA UBINGWA DHIDI YA NORWICH CITY KWA KUIFUNGA MABAO MATATU KWA MBILI

 
Norwich City    2-3Liverpool




Sunday, April 13, 2014

AYA AYA AYA AYA KUMEKUCHAAA

Wale wanaoinua vipaji kipaji ndiyo hiki hapa. kijana pekee mwenye uwezo wa kunyanyua vitu vizito kutokana na uhodari wake aliokuwa nao lakini cha kusikitisha mpaka sasa hajapata mtu wa kumuwezesha kutimiza ndoto zake. Lakini kama tutatazama kwa upande wa pili ni hatari kama atakosa shughuli ya kufanya kwa maana anaweza akawa mkabaji ili akidhi mahitaji yake. wadau mpooo  muwezesheni huyu kijana kabla ajajiwezesha.


CHENGA TUPU

Eti wanasema Elimu ni uhai mbona kila siku wasomi ndiyo wanaongoza kufa alafu sisi mambumbu bado tunatesa tu, hapa asomi mtu!! Gambe kwa kwenda mbelee.
ULEVI NDIYO ULIONIFANYA NIZARAURIKE


Katika maisha yangu sikuwahi kufikiria kuwacha pombe kwakuwa sikuona starehe itakayo nifaa zaidi ya pombe.Wapo wengi niliokuwa nikiwakwaza kutokana na tabia yangu ya ulevi hususa ni wazazi wangu pamoja na ndugu zangu. Kwakuwa nilisha athiriwa na tabia hiyo, ilifika kipindi mpaka sikuona hata umuhimu wa kuwa na mke nakuhisi starehe pekeekwangu ni pombe. Kilichonifanya niache pombe ni hiki:-
Nakumbuka siku moja nililewa sana kiasi ambacho hata kutembea nilikuwa nashindwa, mbaya zaidi ilikuwa ni mida ya saa sita za usiku. Hivyo nilikuwa nikijikokota kuelekea nyumbani kwa ajili ya kupumzika. Lakini sikufanikiwa kufika nyumbani kwa usiku ule kutokana na hali niliyokuwa nayo hivyo nilijikuta nimeanguka chini na kupitiwa na usingizi.
Asubuhi nilivyoamka pombe ilikuwa imeshanitoka hivyo ilinibidi nisimame na kutaka kuanza safari yangu. Kabla sijaondoka eneo lile niliisi kuna utofauti mkubwa katika mwili wangu. Tofauti hizo niliziona hasa sehemu za makalio yangu kwakua kulikuwa kama na majimaji yenye kuteleza. Nilivyojikagua vizuri niliweza kujua yale majimaji yalikuwa ni manii. Hivyo niliweza kubaini kuwa kipindi kile nilichokua nimelala kuna watu walikuja na kuniingilia kinyume na maumbile. Nguvu za miguu ziliniishia ghafla na kuketi chini kwa mda, lakini niliona bora nijikokote na kuelekea nyumbani ili watu wengine wasije kujua kilichonikuta.
Siku nzima nilishinda ndani huku nikiwa na mawazo juu ya tukio nililofanyiwa. Hali hiyo ilinifanya nibadilike na kumrudia mungu wangu na kuachana kabisa na masuala ya pombe.
Baada ya mwezi kupita wadogo zangu wa kiume walikuwa wakijisifia mbele yangu kuwa wao ndiyo walionifanyia mchezo ule wa kunilawiti. Tena walisema tumefanya vile kwa makusudi ili niache pombe. Roho iliniuma sana na nilitamani hata kuwa uwa ndugu zangu. Lakini kadri mazungumzo yalivyokuwa yakiendelea waliniambia ukweli kuhusu tukio lile, kuwa hakuna walichonifanya ila walinimwagia majimaji ya mayai ambayo yanafana na manii.
Sikuamini kwa waliyoyasema lakini ilinibidi ni kubaliane nao kwakuwa sikuwahi kumsimulia yeyote kuhusu yakiyonikuta ila waliniona nimeacha pombe ghafla tu. Sikutaka kuwalaumu kwa walichokifanya ila niliwashukuru kwakuwa ilikuwa kama dawa ya kuacha ulevi kwa upande wangu.

Tuesday, April 1, 2014

CONTACT US

TUNASHUKURU KWA KUTEMBELEA BLOG YETU



KWA USHAURI AU MAONI WASILIANA NASI KUPITIA SIMU NAMBA:+225(0)714025044
                                                                                                                             +225(0)755675362I

AU KUPITIA   E-mail: twalibuissa@gmail.com


endelea kuwa karibu nasi
VIFO VYA WAZAZI WANGU VYANITIA UCHIZI


Ilikuwa ni siku ya mwisho mwa juma {jumapili} nikiwa mimi na baba yangu tulikuwa tukielekea maeneo ya tandale kumtembelea rafiki yake baba ambaye walikuwa wakifanya kazi pamoja. Baba yangu alikuwa akipenda sana kuwa karibu nami kwa kuwa mimi ndiye niliyekuwa mtoto wake wa kike pekee katika familia ya watoto wanne.

Hata nami nilikuwa nikijisikia fahari kuwa karibu na baba yangu na kutembea nae pale anapohitaji. Lakini tukiwa njiani kuelea kwa rafiki wa baba ambaye alikuwa anaitwa Sajali tulikutana na umma wa watu waliokuwa wakishangilia na kuchochea uogomvi kati ya vijana wawili waliokuwa wakigombana. Nilitamani nikawagolezee lakini sikuweza kufanya hivyo kwakuwa nilikuwa sina nguvu ya kuwatawanyisha watu waliokuwa wamewazunguka vijana waliokuwa wakigombana.

Tuliachana na kushangaa tukio hilo kisha tukawa wenye kuendelea na safari yetu. Tulipofika maeneo ya tandale kwa mtogole simu ya baba ilikuwa inaita hivyo ilimbidi aitoe mfukoni kwa ajili ya kuwasiliana. Wakati anatoa simu yake kutoka katika mfuko wa suruali alitokea kijana mmoja na kumgusa bega la kushoto kwa kuashiria kama anamuita.Baba alivyogeuka upande ule wa kushoto ghafla alitokea mtu kwa upande wa kulia na kupola simu ya baba kisha akawa anakimbilia sehemu za vichochoroni. Baba hakutaka kukubali kwa kunyang'anywa simu yake hivyo ilimbidi awakimbize wezi waliomuibia simu yake huku akipiga kelele za wizi.
Kutokana na tukio lililotokea nilipatwa na bumbuwazi {mshangao} nakushindwa kufanya maamuzi ya haraka, baada ya mda kidogo nami nilielekea upande uleule aliokuwa akikimbilia baba alipokuwa akiwakimbiza wale wezi wa simu.

 Lakini kilichonistaaajabisha hakuna mwananchi aliyekuwa akitoa msaada kwa wakati ule ispokuwa walikuwa wakiendelea kufanyanya shughuli zao.Nilipofika mbele kidogo niliona baadhi ya watu wakijitokeza na kushangaa lile tukio. Wasiwasi ulinishika kwa kuwa sikuwa mwenye kujua nini kinaendelea kati ya baba yangu na wale wezi wa simu.  Mara nilisikia kelele za watu wakiitia mwizi kwa upande wa mbele nilipokuwa nikielekea. Ilinibidi niongeze kasi ili nikamsaidie baba yangu.Kumbe zile kelele za wizi nilizokuwa nikizisikia ni wale wezi wa simu wakiwa na wahuni wenziwao walimgeuzia kibao baba yangu na kumuitia kelele za wizi huku wakimtupia mawe.

 Baba yangu aliona njia pekee ya kujitetea ni kukimbilia  maeneo ya barabani, masikini mzazi wangu kumbe kukimbia kwake baadhi ya wananchi wenye hasira kali walifikiri yule ndiye mwizi aliyekuwa ameiba simu.
Hivyo kundi la watu lilimzonga na kuanza kumpiga kwa mawe na magongo. Nilijitahidi kumsaidia baba yangu kwakupiga kelele na kuwaeleza wananchi huyo siyo mwizi bali wamemsingizia lakini hakuna hata mtu mmoja aliyenisikiliza kinyume chake kichapo  kiliongezeka kwa upande wa baba yangu.

Haikuwa rahisi kuamini kile nilichokuwa nikikiona nakuhisi kama mtu niliyekuwa usingizini nikiota. Na kila nilipokuwa nikiomba msaada kwa watu wanisaidie hakuna hata aliyekuwa akinijali. Kutokana na hali hiyo ilipelekea niishiwe nguvu huku nikiwa nalia kwa hasira na machungu makali ya unyama waliokuwa wanaufanya wezi wale.

Baada ya mda askari walipata taarifa hivyo walisogea hadi eneo la tukio kwa lengo la kumkamata muharifu. walimshika baba yangu wakiwa wamembeba na kumpakia katika gari yao. Nilipoangalia pale chini niliona damu imemwagika kwa kiasi kikubwa na kutapakaa eneo la tukio.

Nilirudi nyumbani huku nikiwa nalia njia nzima, nilipofika nyumbani walishangaa kuniona peke yangu kisha huku nikiwa nalia. Ilinibidi niwaelezee kile kilichotokea, Baada ya kujua kilichotokea wote tukawa tunalia huku tukiwa tunaelekea hospitali ya taifa Muhimbili kwa lengo la kujua hali ya baba yangu inaendeleaje.
Kweli tulifanikiwa kufika hospitalini na kujaribu kumuulizia mzazi wetu hodi aliyolazwa. Baada ya kuuliza tulipokea  tarifa kuwa hali ya baba yetu ilikuwa mbaya sana na amelazwa katika chumba cha I C U. Pamoja na hayo hatukuwa wenye kukata tamaa hivyo tulikaa na kusubiri nini kitakacho endelea kwa upande wa mgonjwa wetu.

Baada ya muda kidogo kupita alikuja daktari na kutaka azungumze na mkubwa kutoka katika familia yetu. Hivyo kwa mda ule alijitokeza kaka yetu wa kwanza kwa kuwakilisha familia nzima. Mara baada ya mazungumzo kuisha baina ya daktari na kaka yetu tulimuona kaka akirejea huku machozi yakimtoka na akiwa na huzuni kubwa. Tulivyomuuliza daktari anasemaje  kuhusu mgonjwa wetu, alitujibu kwa sauti ya chini na upole huku akisema baba ameshafariki.

Baada ya kupokea taarifa hiyo ghafla mama alianguka chini kutokana na presha aliyonayo.  Hivyo ilibidi baadhi ya watu watusaidie kumchukuwa mama yetu na kumpeleka kwa daktari kwa ajili ya matibabu.
Kiukweli maamuzi ya mungu ni mazito tena ni makubwa. Kwa maana mda ule ule tukapewa taarifa kuwa mama yetu naye ameiyaga dunia kutokana na mshtuko alioupata.Kitu ninachoamini kazi ya mola huwa haina makosa. Pia sikuwahi kufikiria kutokana na hayo yaliyotokea kwa kudhani kulikuwa na mkono wa mtu ispokuwa ni mitihani tu ya mola wangu.

Namuomba mwenyezi awalaze mahali pema wazazi wangu.

MY DIARY

JOGOO LANGU HALIWIKI 


Leo tupo na bwana Ally ambaye aliweza kusimulia miongoni mwa matatizo aliyowahi kuwa nayo kama ifuatavyo-:

Kwa jina ninaitwa Ally Zola ni kijana mwenye umri wa miaka ishirini na tano {25}. katika maisha yangu hakuna kitu kilichokuwa kinaninyima raha kama kudharaurika na kuonekana kama mtu dhaifu na nisiyekuwa na faida kwa kuumbwa mwanaume eti kwasababu ya mitihani tu ya kimaradhi.

Nakumbuka nilipokuwa na umri wa miaka ishirini {20} nilipatwa na mtihani wa jogoo langu kutowika kabisa kitu ambacho kilikuwa kina ninyima raha na kukosa amani katika maisha yangu. tatizo hili sikuweza kujua ni nini chanzo chake kwani lilinikuta katika mazingira nisiyo ya elewa. kitu ambacho kilinipelekea kuwa na msongo wa mawazo kwa kipindi cha mda mrefu bila ya kujua nianzie wapi kufanya utatuzi wa tatizo langu, hofu yangu kubwa ilikuwa endapo watakapo kuja kujua marafiki zangu kama nimekuwa hanithi niliisi watanifikilia vibaya na hata kunidhania labda nimekuwa shoga.

Hivyo kutokana na hofu hiyo niliyokuwa nayo ilipelekea kudumu na tatizo hilo kwa mda wa miaka miwili bila ya mtu yeyote kujua nasumbuliwa na nini. Lakini nilipofikisha umri wa miaka ishirini na tatu nilishindwa kuvumilia hali hii nikaona bora nianze kutafuta na kuomba ushauri kwa watu wasionijua. Kweli nilipata ushauri tofauti tofauti kutoka kwa watu mbalimbali. Miongaoni mwao walinishauri nitumie baadhi ya miti shamba na wengine walinishauri nijaribu kutumia sana mchuzi wa pweza. kama unavyojua mtu unapokuwa na shida huwa auchagui wa kukusaidia na hata baadhi ya ushauri utakaopewa ili mradi tu ufanikiwe kutatua tatizo lako.

Baada ya kusota kwa mda mrefu bila ya kupata ufumbuzi wa tatizo langu nilikutana na bwana steve ambaye alijaribu kunishauri nikamuone daktari huenda akanisaidia. Nami wala sikupuuzia na kama alivyo nishauri bwana Steve ndivyo nilivyofanya.  Nashukuru nilipo onana na daktari nilimuelezea tatizo langu nae akanipa orodha ya vitu vinavyosababisha tatizo hili.

Alinambia "Uhanithi unawezwa kusababishwa na mambo yafuatayo:-
1. Karibu 50% ya watu wenye tatizo hili husababishwa na umri, msongo wa mawazo n.k.
2. Magonjwa sugu katika mwili, kwa mfano, ugonjwa wa figo, kisukari, kifua kikuu n.k.
3. Matumizi yaliyokithiri ya dawa za kulevya na pombe.
4. Pia vyakula vya mafuta kwani huweza kusababisha mrundikano wa mafuta katika mishipa ya damu na kusababisha mishipa ya damu kushindwa kufika vizuri katika uume ili kuuwezesha kusimama.

Baada ya kujua hayo nilifurahi kidogo na kuwa na hamu pamoja na shauku ya kutaka kujua kama tatizo hili linaweza kutibika au laa.
Daktari alinijibu kwa kusema "kitu cha msingi ni kujua chanzo cha tatizo husika". Na endapo kitakapo bainika chanzo basi utatuzi wake utakuwa rahisi.   Lakini suala la msingi daktari aliniuliza je katika sababu nilizozitaja kuhusu tatizo hili je umeshajua chanzo au sababu ya tatizo lako?  Nilikaa kimya kidogo kwa kufikiri kisha nikamwambia miongoni mwa sababu ulizozita ambazo husababisha tatizo hili mimi nimeangukia katika ulevi wa pombe kupita kiasi.

Baada ya kumueleza hayo daktari aliweza kunishauri na kitu cha kufanya  ili niweze kutatua tatizo langu. Kweli mungu si athumani baada ya kufuata maelekezo ya daktari   kwa muda fulani nilianza kurudisha hali yangu ya kawaida na kupona kabisa na mpka sasa ninamshukuru Mungu nina mke na watoto wawili.    
BARCELONA NAYO YATOA DROO
Timu hiyo ya  Atletico ilijipatia bao lake la kwanza mnamo dakika ya 56 ya mchezo huo. Hata hivyo Barcelona walikuwa wakionekana kuzidiwa kabla ya Diego Costa kutolewa nje ya uwanja kwasababu ya kujeruhiwa. Lakini pia klabu hiyo ya Barcelona iliweza kurudisha bao hilo kataka dakika ya 71. Na mpaka mechi inamalizika hakuna aliyeweza kuongeza bao la pili hivyo Barcelona 1-1 Atletico.
MANCHESTER UNITED YAJIKONGOJA TARATIBU KAMA KOBE
Manchester united yalazimishwa sare na Bayern Munich kwa kufungana gori moja kwa moja (1-1). Lakini pia wakati mchezo huo ukiwa unaendelea mchezaji Bastian Schweinsteiger wa Bayern Munich alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Wayne Rooney.

SPORTS

LIVERPOOL BADO WAPO JUU
Liverpool yaipa kichapo klabu ya Tottenham hotspurs kwa kuifunga mabao 4-0 katika uwanja wa Anfield. Ushindi huo umeifanya liverpool kuwa katika nafasi nzuri kwa kupata alama 71, Alama ambazo zinawafanya wawakaribie wapinzani wao wa klabu ya chelsea kwa kuzidiwa alama mbili.
HAWA NDIYO VIONGOZI WETU


Wananchi: Ndugu muheshimiwa tunaomba tukupe kilio chetu!
Kiongozi: alafu nilie mimi au?
Wananchi: Hapana, utupelekee bungeni.
Kiongozi: Bungeni hakuna msiba....!!!

BEKI TATU ATOA KALI




Mama mwenyenyumba: We Frida mbona hivi vijiti vya kuchokonoa meno vimekwisha haraka?
Dada wa kazi: Mimi mwenyewe sielewi labda uwaulize wanao, mana mimi nikimaliza kuchokonoa meno yangu huwa navirejesha kwenye kikopo chake!!
Mama mwenyenyumba: Heeeee!!!!

INGEKUWA HIVI KILA MTU ANGEJENGA

Baba: We mama miki haya matofali humu ndani yamefuata nini??
Mama: Miki ndiyo aliyoyaleta..!
Baba: Nguvu ya kubeba hayo matofali ameitolea wapi?
Mama: Alikula ile simenti iliyokuwa chini ya kiti sasa ndo amekunya hayo matofali..!!
Baba: Mtume mwananguuu......!!!????

COMEDY

WATOTO WA KIDIGITAL

Mtoto: Baba niletee glasi ya maji
Baba: we mtoto  unakichaa nini? kachukue mwenyewe!
Mtoto: Bwana niletee!
Baba: Usinisumbue, ntakuja kukupiga makofi!
Mtoto: basi ukija kunipiga makofi njoo na glasi ya maji....!

HAYA NI MAONI YA WANANCHI WA KAWAIDA KUTOKANA NA MTAZAMO WAO

Tunashukuru viongozi mbalimbali walioko serikarini na taasisi tofauti tofauti za kidini kwa kupigania haki za kina mama. Pia tunawapongeza hata wakina mama kwa kuliewa jambo kama hili na kuendelea kulitilia mkazo ili kupata usawa baina ya mwanamume na mwanamke. Tena tunasema hongera hata kwa wale waliothubutu kuanzisha vyama au taasisi maalumu zinazo simamia haki za wanawake.
Lakini pia sisi ambao tuko mtaani tunafahamu na kuelewa kuwa lengo kuu la kuanzishwa taasisi au vyama vya wanawake Tanzania kama UWT, MEWATA,TAWLA na vyenginevyo ilikuwa ni kutetea na kupigania haki za wanawake dhidi ya unyanywasaji wa kijinsia na udhalilishwaji uliokuwa ukifanyika kwa upande wa wanawake.
Tunaamini pia taasisi au vyama hivi mpaka kufikia sasa vimefanikiwa kwa kiasi fulani kuweza kuleta mabadiliko na usawa kati ya wanawake na wanamume. Na kitu ambacho kimepelekea kuleta athari kwa upande wa wanawake kama tunavyoshuhudia sasa baadhi ya wanawake wengi hujipa kipao mbele katika kuthubutu kugombania ngazi mbalimbali za uongozi serikalini.
Lakini tuna wasiwasi na mashaka makubwa  kwa kujiuliza maswali yasiyokuwa na majibu sahihi. Kwa mfano miongoni mwa maswali yetu ni kwamba hizi taasisi au vyama hivi vimeanzishwa kwa lengo la kupigania haki za kina mama dhidi ya udhalilishwaji, unyanywasaji na kutaka kumfanya mwanamke apate heshima yake kama watu wengine au taasisi hizi na vyama hivi vimeanishwa kwa lengo na maslahi ya watu fulani???
Tunasema hayo kwakuwa bado tunaona huyu mwanamke aliyekuja kukombolewa na taasissi/vyama hivyo bado anadhalilishwa tena kwa kutembezwa akiwa nusu uchi/uchi kabisa mbele ya hadhara ya watu. Tena cha kusikitisha huwa wanafanya matendo hayo mbele ya watu wazima kama wazazi wao, ni aibu ilioje...??
Tena hupewa majina mazuri kwa kuitwa walimbende(miss) na wanyewe wameridhika kufanya jambo hilo ni kama ajira au njia ya kujiingizia kipato kwa namna moja au nyingine.pia hata baadhi ya viongozi wa kiserikali hualikwa na kuudhuria katika matamasha hayo bila ya wasiwasi.

Embu tazama picha hizi kisha tujiulize je ni kweli taasisi/vyama hivi vimeweza kupinga udhalilishwaji dhidi ya wanawake???


 


Kutokana na ufinyu wa kimawazo kwetu sisi tunaona bado taasisi/vyama hazijafanikiwa katika baadhi ya mambo. Hivyo tunapenda kuzishauri taasisi husika kuendelea kupigania haki za msingi za kina mama bila kubagua, na kama watakusudia kwa dhati watafanikiwa kinyume chake ni kufeli.



NEWS

ONYO
Hii ni kwa wale wanaopenda kukaa na watoto wa watu bila ya kufunga nao ndoa


Kijana mmoja alikua akiishi na msichana ambae kabila lake ni mgita kwa mda wa takribani miaka minne bila ya kumuona na kuishi nae kama mke na mume. Alijikuta analipishwa mahali baada ya msichana aliokuwa akiishi nae kufariki. 
Mzozo ulikuwa siku ya mazishi ya binti huyo ambapo baba mzazi wa msichana yule alimwambia mkwewe atoe faini ya shilingi milioni moja kwakua alikaa na binti yake bila ya kumuoa. Na aliendelea kwa kusema kama akishindwa kulipa pesa hiyo basi maiti hile haitozikwa. Ndugu kwa upande wa mume ilibidi waende kumtaka radhi mzazi huyo ili wazikea.Lakini mzazi huyo alikataa  kabisa na huku akiendelea kudai fedha hizo. Wanandugu kwa upande wa mwanaume ilibidi wamuombe mzee huyo japo wampatie shilingi laki nne badala ya kulipa milioni moja.Baada ya wanandugu wale kuomba kwa mzee huyo, yule mzee alikubali na ndipo mazishi yakafanyika.